Makundi ya Haiti yajaribu kuuteka uwanja wa ndege wa Port-au-Prince


Wanajeshi wamepelekwa ili kulinda uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, dhidi ya kushambuliwa na makundi yenye silaha.


Mashahidi waliripoti kusikia milio ya risasi  karibu na Uwanja wa Ndege wa Toussaint Louverture huku vikosi vya usalama vikikabiliana na watu waliokuwa na silaha nzito.

Lengo la makundi hayo ni kumzuia Waziri Mkuu Ariel Henry kurejea Haiti, ambaye anaaminika kuwa nje ya nchi.
Ghasia zimeongezeka bila kuwepo kwake huku magenge ya watu wakimtaka ajiuzulu.

Bw Henry aliondoka Haiti wiki iliyopita ili kuhudhuria mkutano wa kilele wa kikanda huko Guyana.

Baada ya hapo, alisafiri hadi Kenya kutia saini mkataba wa kutumwa kwa jeshi la polisi wa kimataifa nchini Haiti.

Waziri Mkuu kwa sasa hajulikani aliko lakini msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani alisema: "Tunafahamu kwamba waziri mkuu anarejea nchini [Haiti]".

Akiwa nchini Kenya, muungano wa magenge ukiongozwa na afisa wa zamani wa polisi, Jimmy "Barbecue" Chérizier, ulishambulia shambulia vya polisi na kuvamia magereza makubwa mawili ya Haiti.

Makumi ya watu waliuawa katika shambulio hilo la magereza.

Maelfu ya wafungwa walitoroka na kubaki huru. Mamlaka nchini Haiti imetangaza hali ya dharura ya saa 72.
Previous Post Next Post