Dondoo za Soka Kimataifa

 


Brentford wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Norwich na Marekani Josh Sargent, 24, huku wakijiandaa kwa ajili ya kuondoka kwa mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 27, ambaye anazivutia Chelsea na Arsenal. (Football.London)

Manchester City na Borussia Dortmund wanamfuatilia mshambuliaji wa AC Milan wa timu ya taifa ya Italia chini ya umri wa miaka 17 Francesco Camarda, ambaye anatazamiwa kukataa ofa ya mkataba wa kulipwa katika klabu hiyo ya Serie A atakapofikisha umri wa miaka 16 wiki ijayo. (Gazzetta dello Sport via Football Italia)

Arsenal wamempa kipaumbele mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, 25 msimu huu. (TodoFichajes - kwa Kihispania)

Liverpool wanatazamiwa kuanza mazungumzo na Andy Robertson kuhusu kandarasi mpya msimu huu wa joto na hawana wasiwasi na ripoti zinazomhusisha mlinzi huyo wa kushoto wa Scotland mwenye umri wa miaka 29 na Bayern Munich. (Football Insider)

Baba yake Khvicha Kvaratskhelia anasema winga huyo wa Georgia mwenye umri wa miaka 23 atasalia Napoli msimu huu wa joto licha ya kuhusishwa na Real Madrid na Barcelona. (Radio Serie A via Deportivo )

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot anatazamia kuyapa kipaumbele mazungumzo ya kandarasi mpya na Juventus kuhusu uwezekano wa kuondoka katika klabu hiyo ya Serie A, huku Tottenham wakimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 huku wakitafuta kusaini kiungo wa kati msimu huu. (CaughtOffside)


Liverpool wanatarajia kutengeneza zaidi ya pauni milioni 10 kutokana na filamu ya 'fly-on-the-wall' inayoangazia msimu wa kuaga kwa Jurgen Klopp. (Sun)

Kocha wa zamani wa West Ham Slaven Bilic hayumo kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kuinoa Jamhuri ya Ireland licha ya Mkroatia huyo ambaye kwa sasa anainoa klabu ya Al-Fateh ya Saudi Arabia kuhusishwa na jukumu hilo. (Irish Independent)

Arsenal wanajiandaa kupambana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili mlinzi wa Uhispania Miguel Gutierrez kutoka Girona mwenye umri wa miaka 22. (Fichajes)



Previous Post Next Post